
Zanzibar, 17 Septemba 2025. Mkufunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Koplo Raphael Daudi, ametwaa medali ya dhahabu kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mchezo wa shabaha ya silaha aina ya Pistol kwenye mashindano ya majeshi (BAMATA) yanayoendelea huko Zanzibar.
Ushindi wa kujivunia
Koplo Raphael aliibuka kidedea katika shindano hilo la ulengaji shabaha kwa kutumia Pistol, na kuliletea chuo heshima kubwa katika mashindano hayo ya majeshi ya mwaka 2025.
Pongezi kutoka chuoni
Uongozi na jumuiya ya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam inampongeza Koplo Raphael kwa mafanikio hayo. Ushindi huu unaonyesha umuhimu wa nidhamu, weledi na mazoezi endelevu katika kuimarisha uwezo wa kitaaluma wa askari.

