Chuo cha Polisi Dar es Salaam

Ubora wa Kitaaluma kupitia Mafunzo

Kituo cha Ubora

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Azindua Basi Jipya la Mafunzo ya Udereva wa Abiria (PSV)

Imechapishwa · Na college · dpa news

Dar es Salaam, 25 Septemba 2025. Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Benedict Mambosasa, amezindua basi jipya litakalotumika kwa mafunzo ya udereva wa abiria (PSV) katika shule ya udereva ya chuo, Kilwa Road VTC.

Wito kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari

Wakati wa uzinduzi huo, DCP Mambosasa aliwaasa Maafisa, Wakaguzi na Askari kulinda na kutunza mali na vitendea kazi vya Jeshi. Alisisitiza kuwa utunzaji mzuri wa rasilimali hizo ni sehemu ya uwajibikaji na unachangia ufanisi wa kazi za Jeshi la Polisi.

Kuhusu shule ya udereva ya DPA

Shule ya udereva ya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Kilwa Road VTC Academy Driving School) ilianzishwa kwa lengo la kuzalisha madereva wenye maarifa ya msingi na ujuzi wa vitendo. Mbali na mafunzo ya udereva wa abiria (PSV), shule hii pia hutoa mafunzo ya udereva wa magari makubwa (HGV) na magari ya kawaida.

Msingi wa mafanikio

Kaulimbiu iliyotolewa kwenye hafla hiyo inasisitiza kuwa nidhamu, haki, weledi na uadilifu ndiyo msingi wa mafanikio ya chuo.

Angalia habari zote

Fundisha kwa nidhamu. Tumikia kwa ubora.