Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, tarehe 31 Januari
2024 amefunga rasmi Mahafali ya Saba na Nane ya Vyuo vya Polisi katika
fani mbalimbali za kitaaluma ikiwemo Stashahada na Astashahada ya
upelelzi wa Makosa ya Jinai, Sayansi ya Polisi, Usalama Majini na
Mawasiliano ya Polisi ambapo zaidi ya wahitimu 897 walitunukiwa katika
mahafali hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya
Polisi Kurasini jijini Dar es salaam.