Cheti cha Msingi cha Teknolojia ya Maabara ya Tiba
- NTA Level 4
- Muda Muhula 2 (wiki 34)
Kuhusu programu hii
Programu ina jumla ya wiki 34 za masomo, zilizogawanywa katika mihula miwili. Kila muhula una wiki kumi na tano (15) za mafunzo ya nadharia na vitendo na wiki mbili za mitihani ya mwisho wa muhula. Imesajiliwa na NACTE (Na. REG/PFW/032).
Sifa za kujiunga
- a) Mwombaji anatakiwa kuwa na angalau Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) au sifa inayolingana nacho, akiwa na ufaulu katika masomo ya sayansi, Kemia na Biolojia, daraja D au zaidi.
- b) Ufaulu katika Kiingereza, Fizikia na Hisabati ni faida ya ziada.
Jinsi ya kuomba
- Chuo kwa kawaida hupokea maombi kati ya mwanzoni mwa Desemba na katikati ya Mei ya mwaka kwa ajili ya kozi zitakazoanza mwaka wa masomo unaofuata. Waombaji huomba mtandaoni kupitia NACTE, na waombaji wenye sifa huchaguliwa na NACTE kujiunga na programu hii.

